Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John PiperMfano
Roho Hutusaidia Kufa
Kama umezingirwa kwa jina la Kristo, umebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu na wa Mungu anakukalia. —1 Petro 4:14
Corrie ten Boom anatuambia jinsi alivyokuwa na mashaka kama angeweza kusimama kama angetishiwa na Wajerumani. Alijisikia mnyonge sana alipofikiria kuhusu kinachoweza kutokea. Baba yake, nadhani hivyo, alimpa maelekezo kamili. Alisema, “Unapokuwa unasafiri kwa treni, ninakupa tiketi wiki tatu kabla ya safari au ninakupa unapoingia kwenye treni?" Alijibu, “Ninapoingia kwenye treni.” “Kwa hiyo Mungu atakupa nguvu maalum unayohitaji ili uwe imara unapokabiliana na kufa, na siyo kabla.”
Ninaamini, 1 Petro 4:14 inaahidi kwamba katika nyakati za majaribu makubwa Mungu huja kwa watoto wake na kuwapa nguvu na imani ambayo hawakuijua kama wanaweza. Roho Mtakatifu atakusaidia kufa.
Desturi nzuri inatuambia kwamba Paulo alikatwa kichwa na Nero. Waraka wa mwisho wa Paulo yawezekana ni 2 Timotheo. Hukumu yake tayari ilikuwa imeanza. Pata picha ya askari mzee, akiogopa vita kwa ajili ya Kamanda wake, amefungwa Rumi. Anaitwa mbele ya Mahakama. Kila mtu anajua siku zake zimehesabika. Ni mtu anayejulikana. Na hakuna hata rafiki yake hata mmoja kusimama upande wake. Anajitetea. Uamuzi unafanywa kumsikiliza kwa mara ya mwisho--kisha mwisho. Anarudi kwenye kizimba chake na kuandika maneno hayo kwa Timotheo (2 Timotheo 4:16–17), “Katika jawabu langu la kwanza hakuna aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha. Naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo! Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu.”
Ninaomba kwamba utayakumbuka maneno haya: Roho atakusaidia kufa. Atasimama upande wako wakati hakuna mtu mwingine. Ataiimarisha imani yako. Atakuonyesha utukufu. Atakufanya umtukuze Kristo katika mauti yako. Ujasiri ambao hukuwahi kudhani kwamba utakuwa wako. Roho wa utukufu na wa Mungu atakukalia na kukupeleka nyumbani.
Jifunze zaidi: http://www.desiringgod.org/messages/the-holy-spirit-will-help-you-die
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu
More