Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John PiperMfano
Roho Hutuongoza
Mara kwa mara maandiko yanatusaidia kuelewa changamoto za maisha, ndoa kuvunjika, uasi wa watoto, ulevi wa madawa, vita vya mataifa, kurejea kwa majani msimu wa masika, shauku zisizotoshelezeka za mioyo yetu, hofu ya kifo, kuzaliwa kwa watoto, usawa wa sifa na lawama, kutamalaki kwa kiburi, na pongezi za kujikana.
Biblia inathibitisha asili yake ya kiungu tena na tena kwa kadri inavyoonesha ukweli katika ulimwengu halisi na kutuelekeza njia ya amani. Kwa hiyo, ninatumaini, kwamba moja ya mafundisho tunayoyathamini sana kuyafia (na kuyaishi) ni kwamba Roho Mtakatifu ni mwandishi wa kiungu wa Maandiko yote.
O, kwamba tulikuwa na siku nzima ya kuzungumza kuhusu athari za ajabu za mafundisho haya! Roho Mtakatifu wa milele, Roho wa furaha na upendo kati ya Baba na Mwana, ni mwandishi wa maandiko.
- Kwa hiyo, ni kweli (Zaburi 119:142) na kwa pamoja yanaaminika (Waebrania 6:18).
- Ni yenye nguvu, yakitimiza kusudi lao katika mioyo yetu (1 Wathesalonike 2:13) na hayarudi tupu kwake aliyeyatuma (Isaya 55:10–11).
- Ni safi, kama fedha iliyofuliwa kwenye moto mara saba (Zaburi 12:6).
- Yanatakasa (Yohana 17:17).
- Yanatoa uzima (Zaburi 119:37, 50, 93, 107; Yohana 6:63; Mathayo 4:4).
- Yanahekimisha (Zaburi 19:7; 119:99–100).
- Yanafurahisha (Zaburi 19:8; 119:16, 92, 111, 143, 174) na yanaahidi zawadi kubwa (Zaburi 19:11).
- Yanatoa nguvu kwa wadhaifu (Zaburi 119:28) na yanafariji kwa wenye mashaka (Zaburi 119:76) na hongoza wenye kusumbuka (Zaburi 119:105) na wokovu kwa waliopotea (Zaburi 119:155; 2 Timotheo 3:15).
Hekima ya Mungu kwenye maandiko haimaliziki. Kama elimu hii ni kweli, basi athari zake ni za kuonekana na kufika mbali kwamba kila sehemu ya maisha yetu lazima yaguswe.
Jifunze zaidi: http://www.desiringgod.org/messages/the-holy-spirit-author-of-scripture
Kuhusu Mpango huu
Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu
More