Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John PiperMfano
Roho Hutufanya Salama
Katika yeye...mli...wekwa muhuri wa Roho Mtakatifu, ambaye ni uhakika wa urithi wetu mpaka tutakapopata miliki yake, kwa sifa ya utukufu wake. —Waefeso 1:13-14
Shauku kubwa ya Mungu kwa watu wake ni kutaka wajisikie salama katika pendo lake na nguvu zake. Kila kitu maishani kinaweza kuwa bila msimamo-- afya yetu, familia yetu, kazi yetu, jamii yetu, dunia yetu. Katika viwango hivi vyote unaweza kujisikia kama uko kwenye ghorofa ya arobaini juu kwenye upepo usiotabirika. Unajisikia kama unashindwa kusimama na kuanguka, na kila tofali unalolishika linang'oka.
Kwa kuwa Mungu hufanya mambo kwa ajili ya sifa ya utukufu wake, na kwa kuwa kuliamini neno lake kunatukuza utukufu wake, Mungu huchukua hatua za kujipatia kutukuka kwa utukufu wake milele: anawaweka waamini muhuri wa Roho Mtakatifu, na kuhakikisha kwamba tutakuja katika urithi wetu tukisifu utukufu wake.
Mungu amedhamiria kabisa kuwa na watu wa miliki yake wanaoishi milele kwa sifa ya utukufu wake ambao hataki mustakabali wetu utegemee nguvu zetu za kufanya au kutokufanya. Anamuagiza Roho Mtakatifu kuingia maishani mwetu na kutufanya salama milele.
Mungu alimtuma Roho Mtakatifu kama muhuri kufunga katika imani yetu, kama muhuri wa uthibitisho wa kuthibitisha kuwa sisi ni wana, na kama muhuri wa kulinda dhidi ya nguvu za uharibifu.
Katika Waefeso 1:14, Mungu anasema, “Shauku yangu kuu kwa wale waniaminio ni kwamba ujisikie salama katika pendo langu. Nmekuchagua kabla ya misingi ya dunia. Nimekuchagua toka zamani uwe mwanangu milele. Nimekukomboa kwa damu ya mwanangu. Na nimeweka Roho wangu ndani yako kama muhuri wa uhakika. Kwa hiyo, utapokea urithi na kusifu utukufu wa neema yangu milele na milele.
Na ninakuamba hili katika Waefeso 1 kwa sababu nataka ujisikie salama katika upendo wangu na nguvu zangu. Sikuahidi maisha rahisi. Ukweli, kupitia mateso mengi lazima uingie katika ufalme (Matendo 14:22).Ngoja niseme tena: Nimekuchagua. Nilikuchagua toa awali; nimekuweka muhuri wa Roho wangu. Urithi wako ni wa uhakika, kwa sababu nimedhamiria kuuinua utukufu wa neema yangu katika wokovu wako.”
Jifunze zaidi: http://www.desiringgod.org/messages/sealed-by-the-spirit-to-the-day-of-redemption
Kuhusu Mpango huu
Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu
More