Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John PiperMfano

Live By The Spirit: Devotions With John Piper

SIKU 3 YA 7

Roho Hushinda Hofu

Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamawaga Roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa. —Isaya 44:3

Unajua kwa nini inakuwa rahisi kuwa mwema kwa watu Ijumaa kuliko inavyokuwa Jumatatu? Siyo kwamba ni kwa sababu tumaini ni kama mto unaotiririka kwetu kutoka katika wakati ujao wenye matumaini, na kujaza hifadhi yetu ya furaha, na ndipo hutiririka katika wema kwa wengine?

Ijumaa, mapumziko na burudani viko karibu, na tunaweza kuvionja. Kwa tumaini tunaonja nguvu ya mwisho wa juma ujao. Akiba kidogo ya furaha yetu inaanza kujaa. Na kama mwisho wa juma unaonekana mzuri zaidi, hifadhi yetu ya furaha itajaa na kuanza kumwagika.

Kumwagika huku kwa furaha kuwafikia watu wengine kunaitwa upendo. Kwa hiyo siku zote unakuwa mwema kwa watu unapokuwa na furaha kuhusu yajayo. Tumaini hukujaza furaha, na furaha hufurika kwa tabasamu na maneno mazuri na matendo ya msaada. Inatokea kabla ya likizo, kabla ya kumbukumbu ya kuzaliwa, kabla ya sikukuu, kabla ya Krismasi, na kwa watu wengi, Ijumaa.

Tunapokuwa tumemiminwa na Roho, tunamiminwa na uhakika kwamba Jumatatu zimetengenezwa mbinguni kama Ijumaa. Chochote kinachoonekana cha kutisha kesho hakitakiwi kukutisha kama umejawa na Roho. Mahusiano nyumbani yanaweza kua si mazuri, afya inaweza kuwa inatetereka, mkuu wako wa kazi anaweza kuwa anapanga kukufukuza kazi, kesho inaweza kuleta hali ya kutisha--chochote kinachokufanya uwe na wasiwasi na kesho, fungua moyo wako kwa kumwagika kwa Roho wa Mungu; angalia ahadi zake katika neno lake na atakujaza na tumaini na kuishinda hofu yako.

Wakati Roho Mtakatifu anakuwa amemwagwa, siyo tuu hofu huondoka bali shauku hutoshelezwa pia. Kiu ya nafsi kwa ajili ya Mungu inazimwa-- au angalau tunaonja utoshelevu wa kutosha katika yeye kujua wapi tutaishi maisha yetu yaliyobaki tukinywa.

Maisha yetu ya baadaye yanaweza kunekana giza kwa sababu mbili; ni matarajio kwamba shida inakuja; na nyingine ni matarajio kwamba furaha inakuja. Je, si kweli kwamba moyo wa mwanadamu unasumbuliwa na vitu hivyo; hofu ya shida za baadaye na kiu ya furaha ya baadaye? Kama ndiyo, basi ahadi ya Isaya ndiyo tunayoihitaji; wakati Roho anapomiminwa mioyoni mwetu, hofu hondoka na kiu humalizwa. Nakusihi, basi, kama unatamani kuguswa na Roho wa Mungu katika maisha yako, jitoe usiku na mchana kusoma neno la Mungu.

Jifunze zaidi: http://www.desiringgod.org/messages/a-precious-promise-the-outpouring-of-gods-spirit

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Live By The Spirit: Devotions With John Piper

Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu

More

Tungependa kuwashukuru John Piper na Desiring God kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.desiringgod.org/