Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John PiperMfano

Live By The Spirit: Devotions With John Piper

SIKU 5 YA 7

Roho Hutujaza Furaha

Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima, mkiukomboa wakati, kwa maana zama hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi, bali mjazwe Roho.—Waefeso 5:15-18

Kwa nini watu hupendelea ulevi? Kwa ajili ya furaha. Wote tunapenda kuwa na furaha, lakini kuna tatizo: "siku hizi ni za uovu" (Mstari 16).

Unakimbilia wapi siku zinapokuwa za uovu, unapotishiwa au kukatishwa tamaa au kusongwa na mawazo au wasiwasi? Paulo anatusihi: " Tena msilewe kwa mvinyo; bali mjazwe Roho. Chochote cha thamani ambacho mvinyo unaweza kukuletea, Mungu Roho Mtakatifu anaweza kukupa zaidi."

Kuna watu ambao hawawezi kuanza kupiga mluzi wa furaha au kuimba wimbo kazini kwa sababu wamesongwa na wasiwasi kuhusu maisha. Lakini jioni wakiwa wamepata kinywaji kidogo wanaweza kushikana na marafiki zao na kuimba na kucheka.

Sisi wote tunapenda kuwa huru, kutokufungwa, na wenye furaha. Na hatari kubwa kwa siku zetu, kama Paulo anavyosema, ni kuongezeka kwa watu (hata wakristo) wakiamini kwamba njia pekee ya kupata uhuru huu kama wa mtoto mdogo ni kwa kujiingiza katika ulevi. Tabia kama hizo hazimheshimu Mungu, na ndipo Paulo anasema: Kuna njia bora ya kukabiliana na zama za uovu-- kujazwa na Roho, na utapata furaha isiyo kifani inayokufanya kuimba na kufurahi katika Bwana.

Kwa hiyo, ina maana gani kujawa na Roho?

Roho anayetujaa ni Roho wa furaha inayotiririka daima kati ya Mungu Baba na Mungu Mwana kwa sababu ya kupendezwa na kila mmoja wao. Kwa hiyo, kujawa na Roho maana yake ni kuwa katika furaha ambayo inatiririka katika Utatu Mtakatifu na kumpenda Mungu Baba na upendo uleule wanaopendana wao.

Njia ambayo Roho hupitia katika msitu wa mashaka yetu mpaka kupata furaha ni njia ya imani. Kulingana na Paulo, njia ya kujawa na Roho ni kwa kuamini kuwa Mungu wa tumaini hakika anatawala-- kwamba hakuna hata shomoro aangukaye asipojua Baba (Mathayo 10:29)—na kwamba huendesha dunia kwa ajili yako na wote wanaoamini neno lake. Kwa kuamini hivyo, utajazwa na Roho Mtakatifu na furaha.

Jifunze zaidi: http://www.desiringgod.org/messages/be-filled-with-the-spirit

Andiko

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Live By The Spirit: Devotions With John Piper

Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu

More

Tungependa kuwashukuru John Piper na Desiring God kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.desiringgod.org/