Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

SIKU 12 YA 30

Kazi ya kumshuhudia Kristo katika mazingira yetu si ya kikundi fulani au watu maalumu tu. Ili ujumbe wa Injili uwafikie watu wengi na kwa haraka, yatupasa sote tunaomwamini Yesu Kristo tujitoe na tushirikiane katika kumtangaza huyu kuwa Mwokozi wa ulimwengu kwa njia ya kuwa nuru na chumvi kwa siri na kwa wazi. Yesu mwenyewe anasema hivi: Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni (Mt 5:13-16). Yesu Kristo ametupatia Roho Mtakatifu ili atuwezeshe kusema na kushuhudia kwa nguvu na uweza. Ushuhuda wetu ni muhimu sana kwa sababuwamwiteje yeye[Yesu]wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema(Rum 10:14-15)! Ujihoji, Nimewaleta wangapi kwa Yesu Kristo?

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana