Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

”Huduma ya mauti” inafanywa na sheria ya Mungu, wakati ”huduma ya Roho” inafanywa kupitia Injili ya Yesu Kristo na kuleta wokovu. Mambo makubwa ya huduma hiyo ni haki na uzima, kwa kuwa Roho Mtakatifu ni ”Bwana mtoa uzima” (ndivyo anavyotambulishwa katikaImani wa Nikea, sehemu ya tatu). Kwa imani tunapokea zawadi hizi za haki na uzima. Tunafanywa warithi na raia wa utawala wa Mungu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu kupitia mahubiri juu ya Kristo Yesu, Mwana wa Mungu.Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi(1:19-20).Mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama(3:3).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
