Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Ni wajibu wa viongozi wa jamii kuweka bayana nia na malengo tarajiwa kwa jamii husika. Daudi alifanya hivyo kwa kumweka Sulemani mbele ya watu, kuwa ndiye aliyechanguliwa na Mungu awe mfalme badala yake na kujenga hekalu. Kwa njia hii aliyoichagua Daudi ya kupeleka kwa watu mradi wa ujenzi na mwelekeo wa taifa, tujifunze umuhimu wa washarika wote kushirikishwa mambo ya huduma zinazowakabili. Bila ushiriki kama huo, uchangiaji kwa ajili ya mradi wowote utakuwa dhaifu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz