Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

SIKU 4 YA 30

Moja ya madhaifu ya kanisa la sasa ni kufikiri kwamba kanisa ni kazi au mali ya mtu au viongozi. Twatakiwa tufikiri juu yake kama kazi yaMungu, ambaye ni msanifu mwema na atendaye ipasavyo. Mara moja baada ya kumpa Sulemani mpango mzima wa hekalu, ambao bila shaka aliupata toka kwa Mungu, Daudi anashauri kazi ya kujenga ianze, akimtia mwanawe nguvu. Asiogope, hatakuwa peke yake, Mungu yuko pamoja naye: Uwe hodari, mwenye moyo mkuu, ukatende hivyo; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu, Mungu wangu, yu pamoja nawe; yeye hatakupungukia wala kukuacha, hata itakapomalizika kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya Bwana(m.20). Tutambue kazi ni ya Mungu. Hivyo yuko pamoja nasisikuzotetukimtumikiahata ukamilifu wa dahari(Mt 28:20).

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana