Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

SIKU 7 YA 30

Kitabu cha 1 Nyakati kinaishia kwa ujumbe wa matumaini.“Haya, mhimidini Bwana, Mungu wenu”(m.20). Daudi anaelekeza watu kwa Mungu. Ufalme sio wa Daudi, bali ni wa Mungu. Kiti cha enzi alichokalia Daudi, si chake bali cha Mungu. Mwisho wa utawala wa Daudi sio ndio mwisho wa ufalme wa Mungu. Mungu wake Daudi anabakia katika kiti cha enzi kwenye hekalu lile ambalo atalijenga Sulemani. Baadaye mtoto mwingine wa Daudi ataikamilisha vema kazi hii. Ndiye Yesu. Ndivyo Yesu mwenyewe anasema katika mazungumzo yake na Mafarisayo katika Mt 22:41-46:Yesu aliwauliza,akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.Pianeno la Yesu katika Yn 2:19-21 linathibitisha hivyo:Yesu akajibu, akawaambia[Wayahudi],Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana