Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Kazi ya kitume ambayo Mtume Paulo aliifanya pale Korintho iliambatana na ushirika kati yake na wengine. Katika timu hii ya misheni Timotheo alikuwa na nafasi ya karibu sana na Paulo. Ni Paulo mwenyewe anayethibitisha wazi ushirika huu katika Flp 2:19-20:Natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. Na katika waraka wake wa kwanza kwa Timotheo, Paulo anamsalimu hivi:Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu(1 Tim 1:2). Kazi ya kitume huleta matokeo mazuri ifanywapo kwa upendo na mshikamano. Sasa Paulo anapoandika barua yake, ”watakatifu” wapo nchi yote ya Akaya. Ndio wale wote wanaomwamini na kumtegemea Yesu Kristo. Ndio ”Kanisa la Mungu”. Hali yao hasa ni kuwa chini ya neema na amani ya Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz