1
Mwanzo 32:28
Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza
Yule mtu akamwambia, “Hutaitwa Yakobo tena, bali Israeli, kwa kuwa umeshindana na Mungu na wanadamu, ukashinda.”
Linganisha
Chunguza Mwanzo 32:28
2
Mwanzo 32:26
Kisha yule mtu akamwambia Yakobo, “Niache niende zangu, kwani kunapambazuka.” Lakini Yakobo akamwambia, “Sikuachi kamwe, mpaka umenibariki!”
Chunguza Mwanzo 32:26
3
Mwanzo 32:24
Yakobo alibaki peke yake. Mtu mmoja akaja, akapigana naye mwereka mpaka alfajiri.
Chunguza Mwanzo 32:24
4
Mwanzo 32:30
Yakobo akapaita mahali hapo Penueli, akisema, “Nimemwona Mungu uso kwa uso, nami sikufa.”
Chunguza Mwanzo 32:30
5
Mwanzo 32:25
Mtu huyo alipoona kwamba hawezi kumshinda Yakobo, alimgusa Yakobo nyonga ya kiuno, naye akateguka alipokuwa anapigana naye mwereka.
Chunguza Mwanzo 32:25
6
Mwanzo 32:27
Naye akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akamjibu, “Yakobo.”
Chunguza Mwanzo 32:27
7
Mwanzo 32:29
Ndipo Yakobo akamwambia, “Tafadhali, nakuomba uniambie jina lako.” Lakini yeye akamwambia, “Ya nini kuniuliza jina langu?” Kisha akambariki Yakobo.
Chunguza Mwanzo 32:29
8
Mwanzo 32:10
sistahili hata kidogo fadhili ulizonipa kwa uaminifu mimi mtumishi wako. Nilipovuka mto Yordani, sikuwa na kitu ila fimbo; lakini sasa ninayo makundi haya mawili.
Chunguza Mwanzo 32:10
9
Mwanzo 32:32
Ndiyo maana mpaka leo Waisraeli hawali msuli wa nyonga, kwa maana yule mtu alimgusa Yakobo panapo nyonga katika msuli wa kiuno chake.
Chunguza Mwanzo 32:32
10
Mwanzo 32:9
Kisha Yakobo akamwomba Mungu akisema, “Ee Mungu wa babu yangu Abrahamu, Mungu wa baba yangu Isaka! Ewe Mwenyezi-Mungu uliyeniambia nirudi katika nchi yangu kwa jamaa yangu, ukaniahidi kunitendea mema
Chunguza Mwanzo 32:9
11
Mwanzo 32:11
Nakuomba uniokoe sasa kutoka kwa ndugu yangu Esau, maana nina hofu kuwa atatushambulia na kutuua sote, akina mama pamoja na watoto.
Chunguza Mwanzo 32:11
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video