1
1 Mose 32:28
Swahili Roehl Bible 1937
Ndipo, aliposema: Hutaitwa tena jina lako Yakobo, ila Isiraeli (Mshinda Mungu), kwani umeshindana na Mungu, hata na watu, ukawashinda.
Linganisha
Chunguza 1 Mose 32:28
2
1 Mose 32:26
Akamwambia Yakobo: Niache, niende zangu! Kwani jua limepambazuka. Lakini akasema: Sitakuacha, usiponibariki.
Chunguza 1 Mose 32:26
3
1 Mose 32:24
Naye Yakobo mwenyewe akasalia peke yake ng'ambo ya huko. Mara mtu akakamatana naye, mpaka jua lilipopambazuka.
Chunguza 1 Mose 32:24
4
1 Mose 32:30
Yakobo akapaita mahali pale Penieli (Uso wa Mungu) kwamba: Nimeonana na Mungu uso kwa uso, nayo roho yangu ikapona.
Chunguza 1 Mose 32:30
5
1 Mose 32:25
Alipoona, ya kuwa hamshindi Yakobo, akamgusa nyonga ya kiuno chake; ndipo, nyonga ya kiuno cha Yakobo ilipoteuka kwa kukamatana naye.
Chunguza 1 Mose 32:25
6
1 Mose 32:27
Naye akamwuliza: Jina lako nani? Akasema: Yakobo.
Chunguza 1 Mose 32:27
7
1 Mose 32:29
Naye Yakobo akamwuliza kwamba: Niambie jina lako! Akamwambia: Jina langu unaliulizia nini? Kisha akambariki hapo.
Chunguza 1 Mose 32:29
8
1 Mose 32:10
Hivyo, nilivyo mdogo, sipaswi na magawio yote wala na welekevu wote, uliomfanyizia mtumishi wako. Kwani hapo, nilipouvuka mto huu wa Yordani niliishika hii fimbo yangu tu, lakini sasa ni mwenye vikosi viwili.
Chunguza 1 Mose 32:10
9
1 Mose 32:32
Kwa sababu hii wana wa Isiraeli hawali mshipa ulio juu ya nyonga ya kiuno mpaka siku hii ya leo, kwani yule aliigusa nyonga ya kiuno cha Yakobo penye mshipa wa kiuno.
Chunguza 1 Mose 32:32
10
1 Mose 32:9
Kisha Yakobo akaomba: Mungu wa baba yangu Aburahamu na Mungu wa baba yangu Isaka, wewe Bwana umeniambia: Rudi katika nchi yako kwenye ndugu zako! Mimi nitakufanyizia mema.
Chunguza 1 Mose 32:9
11
1 Mose 32:11
Niponye mkononi mwa mkubwa wangu Esau! Kwani namwogopa, asije, akanipiga mimi na wamama pamoja na wana.
Chunguza 1 Mose 32:11
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video