1
Mwanzo 37:5
Neno: Maandiko Matakatifu
Yusufu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi.
Linganisha
Chunguza Mwanzo 37:5
2
Mwanzo 37:3
Basi, Israeli akampenda Yusufu kuliko yeyote miongoni mwa kaka zake, kwani ni mwanawe wa uzeeni, akamshonea joho lililorembwa vizuri sana.
Chunguza Mwanzo 37:3
3
Mwanzo 37:4
Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yusufu kuliko yeyote mwingine miongoni mwao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema.
Chunguza Mwanzo 37:4
4
Mwanzo 37:9
Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, “Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.”
Chunguza Mwanzo 37:9
5
Mwanzo 37:11
Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni.
Chunguza Mwanzo 37:11
6
Mwanzo 37:6-7
Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.”
Chunguza Mwanzo 37:6-7
7
Mwanzo 37:20
Njooni sasa, tumuue na kumtupa katika shimo mojawapo na tuseme kwamba mnyama mkali amemrarua. Kisha tutaona matokeo ya ndoto zake.”
Chunguza Mwanzo 37:20
8
Mwanzo 37:28
Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yusufu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri.
Chunguza Mwanzo 37:28
9
Mwanzo 37:19
Wakaambiana, “Yule mwota ndoto anakuja!
Chunguza Mwanzo 37:19
10
Mwanzo 37:18
Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga shauri baya la kumuua.
Chunguza Mwanzo 37:18
11
Mwanzo 37:22
Tusimwage damu yoyote. Mtupeni katika shimo lililoko hapa jangwani, lakini msimguse.” Reubeni alisema hivyo ili amwokoe kutoka mikononi mwao, kisha amrudishe nyumbani kwa baba yake.
Chunguza Mwanzo 37:22
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video