Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021Mfano
Ezekieli anapelekwa mpaka kuona mahali patakatifu kuliko kila mahali (41:4). Hamna pazia linalozuia, ila haingii. Kila eneo la hekalu ni takatifu. Lakini kuna chumba kinachoitwa patakatifu, kisha ukiingia ndani zaidi unakuta patakatifu pa patakatifu. Ni hapo akaapo Mungu. Leo tukumbuke Neno linasema miili ya Wakristo ni hekalu takatifu la Roho Mtakatifu, na moyo wako ni patakatifu pa Mungu. Mwenyewe usiingie hapo, bali umwachie Roho wa Mungu akae humo. Hivyo hapatachafuliwa na dhambi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz