1
1 Wafalme 19:12
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Baada ya tetemeko la ardhi moto ukaja, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunong’ona.
Linganisha
Chunguza 1 Wafalme 19:12
2
1 Wafalme 19:4
lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa, Mwenyezi Mungu, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.”
Chunguza 1 Wafalme 19:4
3
1 Wafalme 19:11
Mwenyezi Mungu akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu yu karibu kupita hapo.” Kisha upepo mzito na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la ardhi, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo kwenye lile tetemeko.
Chunguza 1 Wafalme 19:11
4
1 Wafalme 19:13
Ilya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mlango wa pango. Kisha ile sauti ikamwambia, “Ilya, unafanya nini hapa?”
Chunguza 1 Wafalme 19:13
5
1 Wafalme 19:9
Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule. Nalo neno la Mwenyezi Mungu likamjia, kusema, “Unafanya nini hapa, Ilya?”
Chunguza 1 Wafalme 19:9
6
1 Wafalme 19:8
Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini usiku na mchana hadi akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Chunguza 1 Wafalme 19:8
7
1 Wafalme 19:5
Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi. Mara malaika akamgusa na kumwambia, “Inuka ule.”
Chunguza 1 Wafalme 19:5
8
1 Wafalme 19:7
Yule malaika wa Mwenyezi Mungu akaja tena mara ya pili, akamgusa na kumwambia, “Inuka ule, kwa kuwa bado una safari ndefu mbele yako.”
Chunguza 1 Wafalme 19:7
9
1 Wafalme 19:10
Akajibu, “Nimekuwa nikifanya bidii sana kwa ajili ya Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Waisraeli wamelikataa agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi peke yangu niliyebaki, sasa wananitafuta ili waniue pia.”
Chunguza 1 Wafalme 19:10
10
1 Wafalme 19:6
Akatazama pande zote, na hapo karibu na kichwa chake palikuwa na mkate uliookwa kwenye makaa ya moto, na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena.
Chunguza 1 Wafalme 19:6
11
1 Wafalme 19:2
Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Ilya, kusema, “Miungu waniadhibu vikali zaidi, ikiwa kesho wakati kama huu sitakuwa nimeondoa uhai wako kama mmoja wa hao manabii.”
Chunguza 1 Wafalme 19:2
12
1 Wafalme 19:18
Hata sasa nimeweka akiba ya watu elfu saba katika Israeli, wote ambao hawajampigia Baali magoti, na wote ambao midomo yao haijambusu.”
Chunguza 1 Wafalme 19:18
13
1 Wafalme 19:19
Hivyo Ilya akaondoka huko na kumkuta Al-Yasa mwana wa Shafati. Alikuwa akilima kwa jozi kumi na mbili za maksai, na yeye mwenyewe aliiongoza ile jozi ya kumi na mbili. Ilya akamwendea, na kumvisha vazi lake.
Chunguza 1 Wafalme 19:19
14
1 Wafalme 19:21
Basi Al-Yasa akamwacha Ilya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Ilya, akamtumikia.
Chunguza 1 Wafalme 19:21
15
1 Wafalme 19:20
Kisha Al-Yasa akawaacha maksai wake, akamkimbilia Ilya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.” Ilya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekufanya nini?”
Chunguza 1 Wafalme 19:20
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video