1
Mwanzo 37:5
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Yusufu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi.
Linganisha
Chunguza Mwanzo 37:5
2
Mwanzo 37:3
Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko ndugu zake wote, kwa sababu alikuwa mwanawe wa uzeeni; akamshonea joho lililofumwa vizuri sana.
Chunguza Mwanzo 37:3
3
Mwanzo 37:4
Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yusufu kuliko yeyote kati yao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema.
Chunguza Mwanzo 37:4
4
Mwanzo 37:9
Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akisema, “Sikilizeni: nimeota ndoto nyingine. Wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.”
Chunguza Mwanzo 37:9
5
Mwanzo 37:11
Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni.
Chunguza Mwanzo 37:11
6
Mwanzo 37:6-7
Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani. Ghafula mganda wangu ukasimama wima, nayo miganda yenu ikauzunguka na kuuinamia.”
Chunguza Mwanzo 37:6-7
7
Mwanzo 37:20
Njooni sasa, tumuue na kumtupa katika shimo mojawapo, na tuseme kwamba mnyama mkali amemrarua. Kisha tutaona matokeo ya ndoto zake.”
Chunguza Mwanzo 37:20
8
Mwanzo 37:28
Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yusufu kutoka lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri.
Chunguza Mwanzo 37:28
9
Mwanzo 37:19
Wakaambiana, “Yule mwota ndoto anakuja!
Chunguza Mwanzo 37:19
10
Mwanzo 37:18
Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga njama za kumuua.
Chunguza Mwanzo 37:18
11
Mwanzo 37:22
Msimwage damu yoyote. Mtupeni katika shimo lililoko hapa jangwani, lakini msimguse.” Reubeni alisema hivyo ili amwokoe kutoka mikononi mwao, kisha amrudishe nyumbani mwa baba yake.
Chunguza Mwanzo 37:22
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video