1
1 Fal 17:14
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi.
Linganisha
Chunguza 1 Fal 17:14
2
1 Fal 17:1
Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.
Chunguza 1 Fal 17:1
3
1 Fal 17:13
Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.
Chunguza 1 Fal 17:13
4
1 Fal 17:12
Naye akasema, Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.
Chunguza 1 Fal 17:12
5
1 Fal 17:9
Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.
Chunguza 1 Fal 17:9
6
1 Fal 17:16
Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya.
Chunguza 1 Fal 17:16
7
1 Fal 17:15
Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi.
Chunguza 1 Fal 17:15
8
1 Fal 17:10
Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.
Chunguza 1 Fal 17:10
9
1 Fal 17:4
Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko.
Chunguza 1 Fal 17:4
10
1 Fal 17:11
Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako.
Chunguza 1 Fal 17:11
11
1 Fal 17:6
Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.
Chunguza 1 Fal 17:6
12
1 Fal 17:7
Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.
Chunguza 1 Fal 17:7
13
1 Fal 17:24
Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la BWANA kinywani mwako ni kweli.
Chunguza 1 Fal 17:24
14
1 Fal 17:5
Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani.
Chunguza 1 Fal 17:5
15
1 Fal 17:22
BWANA akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka.
Chunguza 1 Fal 17:22
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video